Mashirika ya Biashara

Uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabianchi ni mbili kati ya changamoto kubwa zaidi za wakati wetu lakini zinaandaa pia fursa ya kufanya vizuri zaidi.

Sekta ya kibinafsi, yenye ubunifu usioisha na inayochochea badiliko iko katika hali nzuri kuchangia ubora wa hali ya hewa. Kwa kutoa suluhu na kubunu teknolojia zinazotoa kiwango kidogo cha uchafu, bidhaa, na huduma, biashara zinaweza kusaidia kusawazisha tena uhusiano kati ya wanadamu na mazingira, na kuhakikisha hewa safi kwa watu wote.

Kampeni Yetu

Baraza la Kiuchumi la Ulimwengu limeshirikiana na Shirika la Mazingira la UN ili kuhusisha sekta ya kibinafsi na kuchochea uwajibikaji kupitia Muungano mpya kwa Ajili ya Hewa Safi. Septemba 7, Baraza hilo litakuwa na mazungumzo na viongozi na wataalamu wa sekta, wakizungumzia fursa za kupunguza uchafuzi wa hewa; na mazoea bora yataangaziwa, katika mwaka mmoja ujao.

Septemba 7 mwaka huu– maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu– yanaazimia kupunguza uchafuzi na kuwekeza katika utafiti na maendeleo ili kuwazia njia mpya za kufanya biashara.

Jifunze mengi zaidi kuhusu mambo ambayo biashara inaweza kufanya ili kusaidia kufanikisha #HewaSafiKwaWote, hapa.