Ripoti na Machapisho

Ili kuibuka washindi katika katika vita vyovyote, ni sharti kumfahamu adui yetu. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa  na wabia wake, kama vile Shirika la Afya Duniani , wanatoa taarifa mpya mara kwa mara kuhusu uchafuzi wa hewa na kufanya utafiti wa kupelekea masuluhisho mapya. Soma ripoti kupitia linki zilizopo hapo chini ujifahamishi zaidi ili uweze kuchukua hatua mwafaka. 

Tathmini ya Kwanza ya Kimataifa ya Sheria za Uchafuzi wa Hewa

Tathmini ya Kimataifa ya Sheria za Uchafuzi wa Hewa (GAAPL) inawasilisha matokeo ya utafiti wa sheria za ubora wa hewa katika nchi 194 na katika Umoja wa Ulaya. Kwa kutumia Miongozo ya Ubora wa Hewa iliyoandaliwa na Shirika la Afya Duniani kama mahali pa kuanzia, ripoti hiyo inachunguza hatua za…

Hatua Kuhusu Ubora wa Hewa: Muhtasari wa Kimataifa wa Sera na Programu za Kupunguza Uchafuzi wa Hewa

Ripoti hii mpya inatokana na data iliyokusanywa mwaka wa 2020 kupitia utafiti wa wa kina ulioshirikiwa na nchi wanachama, na kujumuisha machapisho mwafaka inayoonyesha hatua muhimu zinazochukuliwa na serikali kote ulimwenguni kuboresha hali ya hewa. Ripoti hii inakamilishwa na mihtasari za kikanda…