Kaulimbiu

#PamojaKuwaNaHewaSafi

Kaulimbiu ya mwaka huu ya “Pamoja Kuwa na Hewa Safi” inaangazia umuhimu wa kuwa na ushirikiano imara, kuimarisha uwekezaji, na kushirikiana kuwajibika ili kukabiliana na uchafuzi wa hewa. Hali ya kuvuka mipaka ya uchafuzi wa hewa inahitaji ushirikiano wa kimataifa na hatua za pamoja kutoka kwa washikadau wote. Inafuatia kaulimbiu ya mwaka wa 2022 ya " Hewa Yetu Sote".

Uchafuzi wa hewa sasa ndilo tishio kubwa zaidi la mazingira kwa afya, likisababisha vifo vya mapema vya takriban watu milioni 7 kila mwaka vinavyotokana na magonjwa kama vile kiharusi, ugonjwa wa moyo, ugonjwa sugu wa mapafu, saratani ya mapafu na maambukizi makali ya mfumo wa kupumulia. Vyanzo vingi vya uchafuzi wa hewa pia husababisha mabadiliko ya tabianchi na huharibu mazingira na mifumo ya ekolojia. Uchafuzi wa hewa huathiri vibaya utoshelezaji wa chakula, usawa wa kijamii na kijinsia, na maendeleo ya kiuchumi, na kudumisha watu katika maisha ya umaskini.

Janga la COVID-19 limedhihirisha tishio la uchafuzi wa mazingira. Takwimu zimetolewa zinazoonyesha kuwa uchafuzi huenda unawaweka watu katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya COVID-19 .

Hewa safi itatufanya kuwa na afya bora zaidi, italinda mazingira, kusaidia kufikia malengo ya mabadiliko ya tabianchi duniani, kuimarisha ubora wa maisha na kuandaa siku zijazo salama na zenye usawa kwa wote. Tukichukua hatua sasa, tunaweza kupunguza kwa nusu uharibifu wa mimea duniani kutokana na vichafuzi hivi kufikia mwaka wa 2050. Kupunguza uzalishaji wa methani, inayochangia gesi ya ukaa na kuchafua hewa, kunaweza kuokoa kati ya Dola za Marekani bilioni 4 na bilioni 33.

Tushirikiane nyumbani na katika sehemu zetu za kazi, katika jamii, serikalini na mipakani kuboresha hewa yetu. 

Sisi sote tuna haki ya kuvuta hewa safi. Pamoja tunaweza kuhakikisha ujumbe wa maadhimisho ya nne ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za bluu unakuwa wito wa kimataifa wa kuchukua hatua zitakazoleta mabadiliko ya kudumu ili kuhakikisha vizazi vijavyo vinavuta hewa safi.

Tuna masuluhisho ya kukomesha uchafuzi wa hewa, na ni lazima lazima tuchukue hatua zinazohitajika kuhakikisha kuwa uchafuzi wa hewa hautakuwa tatizo kwetu zote katika siku zijazo. 

Watu wanaweza kushiriki maoni yao kuhusu Hewa Safi ili kuwa na anga za bluu kwa kushiriki juhudi zao kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia hashitagi #PamojaKuwaNaHewaSafi na #SikuyaHewaSafiDuniani.