Majiji

Zaidi ya nusu ya idadi ya watu ulimwenguni huishi katika majiji leo. Mali muhimu zaidi ya jiji ni afya ya raia zake. Licha ya hilo, zaidi ya asilimia 80 ya watu wanaoishi kwenye majiji huathiriwa na viwango vya uchafuzi wa hewa vinavyozidi vya miongozo ya Shirika la Afya Ulimwenguni na asilimia 98 ya majiji katika maeneo yenye mapato ya chini huathiriwa na hewa mbaya. Pasipo kuchukua hatua madhubuti, uchafuzi wa hewa katika majiji mengi utaendelea kuwa mbaya zaidi na mabadiliko ya tabianchi yataongezeka hata zaidi.

Kampeni Yetu

Ulimwenguni kote, majiji yanawajibika kufikia Miongozo ya Ubora wa Hewa ya WHO kufikia 2030. Majiji yanaweza kuchangia sehemu muhimu katika vita dhidi ya uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabianchi – kwa kubuni sera na programu zinazozuia uchafuzi na kuchochea matumizi ya nishati isiyochafua mazingira, na kuetekeleza hatua ya kitaifa ili kuzuia uchafuzi wa hewa kutoka katika vyanzo vilivyo nje ya eneo la mji.

Inajumuisha jitihada kupitia #BreatheLife, kuazimia kutenda kupitia mpango ulioanzishwa na Umoja wa Mataifa wa Hewa Safi, na kutumia mitandao kama vile C40, ICLEI, World Resources Institute, World Wildlife Fund, Global Covenant of Mayors , Clean Air Asia, Clean Air Institute ili kuchochea hatua za kufikia suluhisho linalofaa.

Mnamo Septemba 7 mwaka huu katika maadhimisho ya kwanza – Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu – pata habari kuhusu  ubora wa hewa katika jiji lako na hatua zinazoweza kuchukuliwa na jiji lako ili kupunguza uchafuzi wa hewa.

Jifunze mengi zaidi kuhusu mambo ambayo majiji yanaweza kufanya ili kufikia #HewaSafiKwaWote, hapa.

Pitia kwenye ramani hii uone kinachofanywa na miji kukabiliana na uchafuzi wa hewa 

Video zisizo za Umoja wa Mataifa zinazoangiwa hapa zilipokelewa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kutoka kwa wabia ili kuunga mkono Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na mawingu ya bluu. UNEP siyo chanzo cha makala hayo. Kujumuishwa kwake hapa haimanishi uidhinishaji wa matukio au makala ndanimwe. 

Michoro imetoka kwa serikali au imepatikana kupitia Creative Commons License