Hewa Safi na SDGs

 

Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanalenga kumaliza umaskini uliokithiri na kuunda ulimwengu safi na endelevu kufikia mwaka mwa 2030. Katika msingi wake kuna afya na ustawi wa watu na sayari yetu, ambayo inamaanisha uchafuzi wa hewa-vifo na ulemavu unaosababisha na uhusiano wake wa karibu na mabadiliko ya tabianchi-ni tishio kubwa la kutimiza maono ya ulimwengu bora. Hata hivyo, malengo pia yanaweza kutumika kama silaha dhidi ya uchafuzi wa hewa. Kwa njia hii:

Lengo 3 linalenga afya njema na ustawi kwa wote — nguzo ya kuwezesha watu kufikia malengo yao shuleni, kazini na nyumbani. Kila hatua tunayochukua kukabilisns ns uchafuzi wa hewa ni hatua kuelekea kufikia lengo hili.

Lengo la 7 linalenga upatikanaji wa nishati isiyochafua mazingira kwa bei nafuu- ambayo ni muhimu kwa kuondoa watu kutoka kwenye umaskini na kuwezesha maendeleo endelevu ya uchumi. Watu bilioni tatu wanapika na kupasha joto nyumba zao na fueli inayochafua mazingira. Uchafuzi wa hewa unaofuata unaua karibu watu milioni 4 kila mwaka, haswa wanawake na watoto. Nishati isiyochafua mazingira na inayoweza kutumika tena itaokoa maisha na kukuza maendeleo ya uchumi.

Lengo la 11 la miji na jamii endelevu ni muhimu katika ulimwengu wetu wa miji. Mwaka wa 2016, zaidi ya nusu ya wakaazi wa mijini walishuhudia uchafuzi wa hewa wa nje angalau mara 2.5 zaidi kuliko viwango salama vya Shirika la Afya Duniani. Sera zinazofanya miji kuwa nadhifu, thabiti na ya kijani kibichi — kupitia kupanga miji, teknolojia na ushiriki wa raia — inaweza kutoa hali bora ya hewa na kubadilisha mazingira ya mijini.

Lengo 13 linashughulikia mabadiliko ya tabianchi. Vichafuzi vingi vya hewa vinavyoathiri afya zetu pia huongeza joto kwenye anga. Vitendo vya kuboresha ubora wa hewa-kama vile kuanza kutumia nishati isiyochafua mazingira, suluhisho la upishi na uchukuzi-pia zitashughulikia dharura ya hali ya hewa.