15 September 2020 Siku ya Ozoni Duniani ya Mwaka wa 2020 – Ozoni milele!

Kutokana na ushirikiano wa kimataifa, mwaka huu tunaadhimisha miaka 35 ya Mkataba wa Vienna  na miaka 35 ya kutunza tambiko la ozoni.

Video

Septemba 16, ni Siku ya Ozoni Duniani. Kutokana na ushirikiano wa kimataifa, mwaka huu tunaadhimisha miaka 35 ya Mkataba wa Vienna  na miaka 35 ya kutunza tambiko la ozoni.

 Siku ya Ozoni Duniani inaonyesha maamuzi yanayochukuliwa kwa ushirikiano huku yakiongozwa na sayansi, ndiyo njia ya pekee ya kusuluhisha majanga makuu duniani.

 

Utangulizi:

Mnamo mwaka wa 1985, serikali ulimwenguni ziliidhinisha Mkataba wa Vienna  wa Kutunza Tambiko la Ozoni. Kwenye Protokali ya Montreal  Chini ya mkataba huo, serikali, wanasayansi na wamiliki wa viwanda walishirikiana kupunguza matumizi ya vitu vinavyoathiri ozoni kwa asilimia 99. Kutokana na Mkataba wa Vienna , tambiko la ozoni linaendelea kuimarika na linatarajiwa kurudi kama lilivyokuwa kabla ya miaka ya 1980 kufikia katikati mwa karne. Ili kuunga Protokali hiyo mkono, Marekebisho ya Kigali, ya mwaka wa 2019, yanalenga kupunguza hydrofluorocarbon (HFCs), gesi ya ukaa iliyo na uwezekano mkubwa wa kuongeza kiwango cha joto duniani na kuharibu mazingira.

Recent Stories
Toleo la habari

Matukio ya hali mbaya zaidi ya uchafuzi wa hewa yanapoendelea kuongezeka, juhudi za kimataifa za kupunguza uchafuzi wa hewa na athari zake…

Toleo la habari

Matukio ya hali mbaya zaidi ya uchafuzi wa hewa yanapoendelea kuongezeka, juhudi za kimataifa za kupunguza uchafuzi wa hewa na athari zake…