26 November 2019 Mambo 10 unayopaswa kufahamu katika Ripoti ya mwaka wa 2019 ya Hatua Zilizosalia Kupunguza Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu

Ripoti inayotolewa kila mwaka na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ya Hatua Zilizosalia Kupunguza Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu sasa inapatikana mtandaoni. Je, lakini ripoti hii inahusu nini? Na inatuhusu vipi? Endelea kusoma ili kujifahamisha zaidi. 

Tukio

Ripoti inayotolewa kila mwaka na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ya Hatua Zilizosalia Kupunguza Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu sasa inapatikana mtandaoni. Je, lakini ripoti hii inahusu nini? Na inatuhusu vipi? Endelea kusoma ili kujifahamisha zaidi. 

1. "Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu" ni nini?

image
Picha na Pixabay

"Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu" maarufu kama “Emissions Gap” linaweza kutambulika pia kama "Pengo kwenye ahadi"  Hutathmini pengo kati ya yale tunayohitaji kufanya na yale hasa tunayofanya ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pengo ni tofauti iliopo baada ya kulinganisha kiwango kidogo cha uzalishaji wa gesi chafu kinachohitajika duniani na kiwango kinachotarajiwa kupunguzwa kwa kuzingatia ahadi za nchi za kukabiliana na gesi ya ukaa.

2. Umuhimu wa Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu ni upi? 

image
Picha na UNEP

Pengo hili ni muhimu kwa sababu iwapo hatutalipunguza na kufikia malengo ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafu, tutashuhudia athari mbaya mno za mabadiliko ya tabianchi kote duniani. Ni muhimu kwa waunda sera na wananchi kufahamu kuhusu pengo hilo ili kuwajibisha nchi zijitolee vya kutosha kupunguza pengo hilo.

3. Ripoti ya Hatua Zilizosalia Kupunguza Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu hutathmini nini? ?

image
Picha na Pixabay

Ripoti hii inayotolewa kila mwaka na UNEP hutathmini nchi zilizoweka hatua za kupunguza pengo zimefikia wapi kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa lengo la kukomesha mabadiliko ya tabianchi. 

Ripoti ya Hatua Zilizosalia Kupunguza Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu hutathmini mienendo mikuu mitatu:  

  1. Kiwango cha uzalishaji wa gesi ya ukaa kila mwaka hadi mwaka wa 2030
  2. Kujtolea kwa nchi kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na athari zinazoweza kutokea kutokana ahadi za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa jumla.
  3. Kiwango kinachohitajika ili kuwa na uzalishaji mdogo wa gesi chafu utakaoweza kudhibiti kiwango cha joto kuwa nyuzijoto 1.5 na kwa gharama isiyokuwa ghali.

Pia, ripoti inaorodhesha mambo muhimu yanayostahili kuzingatiwa na kila nchi ili kuongeza kasi ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa lengo la kupunguza pengo lililopo.

4. Tunaendelea vipi? 

image
Kutoka UNEP

Kwa kipindi cha miaka kumi ya kuandaa Ripoti ya Hatua Zilizosalia Kupunguza Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu, pengo kati ya yale tunayohitaji kufanya na yale hasa tunayofanya bado ni kubwa kama kawaida.    

Tunapokaribia mwaka wa 2020, tunapaswa sasa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 7.6 kila mwaka tangu mwaka wa 2020 hadi mwaka wa 2030. Tusipofaulu kufanya hivyo hatutafaulu kufikia nyuzijoto 1.5 zinazolengwa. Tusipochukua hatua dhidi ya hali iliopo na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kiwango cha joto kinatarajiwa kuongezeka kwa nyuzijoto 3.2 zaidi ya kiwango cha kawaida na kusababisha madhara mabaya zaidi kwa mazingira.   

5. Kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kila mwaka una manufaa yepi? 

image
Source: UNEP Emissions Gap Report 2019

Miaka kumi iliyopita, iwapo nchi zingeshughulikia suala hili, serikali zingehitaji kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 3.3 kila mwaka. Kwa sasa, tunahitaji kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 7.6 kila mwaka. Kufikia mwaka wa 2025, tunahitaji kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 15.5 kila mwaka. Kila siku tunapochelewa kuchukua hatua, ndipo itakapokuwa vigumu kabisa na ghali mno kupunguza uzalishaji wa gesi chafu. Jifahamishe zaidi hapa

6. Uzalishaji wa gesi chafu hutoka wapi?

image
Kutoka: UNEP Emissions Gap Report 2019

Nchi wanachama wa G20 huzalisha asilimia 78 ya gesi chafu duniani lakini nchi saba hazijaweka sera au mikakati ya kuziwezesha kutekeleza ahadi zao chini ya Mkataba wa Paris. Wazalishaji wakuu wanne (China, Marekani, EU28 na India) wamechangia zaidi ya asilimia 55 ya uzalishaji wa hewa chafu kwa jumla kwa kipindi cha karne iliyopita, bila kujumuisha uzalishaji kutokana na mabadiliko kwa matumizi ya ardhi kama vile ukataji wa miti. Tukijumuisha uzalishaji wa hewa chafu kutokana na mabadiliko kwenye matumizi ya ardhi, takwimu zitabadilika huku kukiwa na uwezekano wa Brazil kuwa mzalishaji mkubwa. Kiwango kikubwa cha uzalishaji kinatokea katika sekta ya nishati kutokana na matumizi ya visukuku. Viwanda huchukua nafasi ya pili kama wazalishaji wakubwa wa gesi chafu, vikifuatiwa na sekta za misitu, usafiri, kilimo na sekta ya ujenzi. Jifahamishe zaidi hapa.

7. Je, kuna uwezekano wa kupunguza pengo hili? Naam, inawezekana!      

image
Picha na Pixabay

Kuna uwezekano wa kudhibiti mabadiliko ya tabianchi kuwa nyuzijoto 1.5. Ni sharti tupunguze uzalishaji wa gesi chafu mara dufu kufikia mwaka wa 2030—hii inamaanisha uzalishaji wa hewa chafu sharti upungue kwa asilimia 7.6 kila mwaka  kuanzia mwaka wa 2020. Habari njema ni kuwa tuna teknolojia na sayansi itakayotuweza kuepukana na hewa ya ukaa katika sekta ya nishati, ya usafiri na katika miji yetu. Tuna elimu tunayohitaji ili kukomesha ukataji wa miti na kuimarisha upandaji wa miti. Na haya yote yanaweza kupatikana kwa bei nafuu.  Tunachohitaji tu ni kujitolea. Kujitolea kwa serikali kwa ushirikiano na wananchi wao.

Kwa bahati nzuri, manufaa anuai ya kushughulikia mazingira yanaendelea kueleweka kwa kasi -kwa mfano kuwa na hewa safi, kuimarisha afya, kuwa na miji safi inayotumia kawi kikamilifu na kuongezeka kwa matumizi ya nishati jadidifu.   Kuchukua hatua na kujitolea kuzitekeleza kunaongezeka kwa kasi sawia na kuongezeka kwa uelewaji huu.

8. Je, tunahitaji nini kupunguza pengo lililopo?

image
Picha na Unsplash

Kukabiliana kabisa na hewa ya ukaa katika sekta ya nishati ni suala muhimu linalowezekana. Nishati jadidifu na nishati isiyotumia nguvu nyingi za umeme ni muhimu ili kuleta mabadiliko katika sekta ya nishati. Kuna uwezekano wa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa gigatani 12.1 kufikia mwaka wa 2050 kwa kutumia nishati jadidifu. Hii ni sawia na matumizi ya kila mwaka ya takribani milioni mbili hunusu ya makaa ya mawe kuzalisha nguvu za umeme: zaidi ya ilivyo duniani  kwa sasa. Kutumia vyombo vya usafiri vinavyotumia nguvu za umeme kunaweza kupunguza uzalishaji wa kaboniksidikwa kiwango kikubwa cha asilimia 72 kufikia mwaka wa 2050. Kila sekta na kila nchi ina fursa ya kipekee ya kutumia nishati jadidifu, kutunza malighafi, kulinda maisha na vipato, na kuepukana na matumizi ya vitu vinavyozalisha hewa ya ukaa.

9. Ni nini haswa kinachofanywa na nchi yangu?

image
Picha na Pixabay

Angalia ni nchi zipi zina ahadi nyingi za kipekee kufikia sasa na ni nchi zipi zimetoa ahadi mpya hivi karibuni. Je taifa lako ni nchi mwanachama wa G20? Soma uchanganuzi na mapendekezo yetu kwa upana hapa ya fursa kuu zilizopo zilizo na uwezo wa kufanya ni nchi mwanachama wa G20 kuepukana na hewa ya ukaa kwa kasi.

10. Ni nini ninachoweza kufanya? Iwapo huna mda, soma habari zetu za kuathiri au tazama video yetu. Kwa taarifa na mapendekezo kwa kina, tafadhali soma ripoti hiyo. Na, uelimike zaidi, shiriki na uwasihi waunda sera kuchukua hatua sasa.

 

 

Recent Stories
Video

Kutokana na ushirikiano wa kimataifa, mwaka huu tunaadhimisha miaka 35 ya Mkataba wa Vienna  na miaka 35 ya kutunza tambiko la ozoni.

Toleo la habari

Matukio ya hali mbaya zaidi ya uchafuzi wa hewa yanapoendelea kuongezeka, juhudi za kimataifa za kupunguza uchafuzi wa hewa na athari zake…